The lead Jicho Pevu , a hawk-eyed reporter with KTN has written a letter to the president advising him on the course to take after the recent attack which led to several KDF soldiers dying.
Among the, he is advising Uhuru to sent top officials to go on the ground. Find out more details below.
“Naomba uwaregeshe wanajeshi wetu nyumbani. Ombi langu linatokana na sababu tasa za Kenya kuwatuma nchini Somalia. Kwanza hatuna sababu za kupigana nao kwa sababu hamna chochote tunachopigania wala kupata huko Somalia. Amerika inapovamia taifa lingine hufanya hivyo kwa misingi ya maslahi na wala sio demokrasia. Aidha inashambulia taifa lingine kwa sababu ya mafuta, eneo la kuweka wanajeshi wake kwa mafunzo na kambi au njia ya kuuza silaha zao. Kama kuna wanafiki wakubwa dunia hii ni wamarekani na wachumba zao Israel na Uingereza. Ni kwa nini vijana wetu wauawe kinyama kila kukicha kwa ajili ya makosa ya marekani? Kuingia kwa wanajeshi wa Kenya Somalia kulitokana na kutekwa nyara kwa ajuza mmoja mtalii huko Lamu na Alshabab. Jeshi liliamua kuingia Somalia kwa sababu za ajuza huyo na wala sio wakenya wanaouawa na kutekwa nyara kila mara na Alshabab. Tamaa ya pesa pia imechangia pakubwa. Yaani wanasiasa na baadhi ya wakuu wa jeshi waliokuwa hapo awali waliona ni vyema kula pesa za wanajeshi hao huku wao wakihangaika kutulinda sisi. Hakika jeshi limegeuzwa na kuwa kama polisi. Hii sio jeshi ya Daniel Toroitich Arap Moi tuliyokuwa tukiiheshimu na kuienzi. Wakuu wa jeshi wamekuwa wakabila wakubwa wanaojiingiza kwa mambo ya kisiasa. Uhuru Kenyatta warudishe ndugu na dada zetu nyumbani maana tumechoka kulia. Kama amerika ina shida, waende wao wakapigane nao. El Adde mlitudang’anya eti mliwashambulia kabla ya Alshabab kutoa kanda ya video na kutuonyesha jinsi ambavyo waliwaangamiza watoto wetu. Hii ya ijumaa iliyopita mmetudang’anya lakini kwa vile jeshi pia limeanza tabia za polisi wakenya watasubiri kuona kanda ya Alshabab maana hawaamini serikali yao. Mwisho kabisa kama unaona ni uzalendo kwa wao kubakia naomba uwatume vijana wako, kila waziri ndani ya serikali yako atume vijane wake, mkuu wa jeshi atume kijana wake na hao wanasiasa wanaopayuka kila kukicha ndani ya bunge, seneti na kupasisha mijadala za kitoto pia watume watoto zao. Mkifanya hivyo nitajua ni ukenya na uzalendo nami pia nitajitolea kuungana nao kulinda taifa langu Kenya,” Mohammed Ali wrote in part.